IMELETWA KWAKO NA SIMULIZI MIX ENTERTAINMENT
MWANDISHI ZUBERY RAZUUR MAVUGO.
SEHEMU YA NNE .
ILIPOISHIA:
‘’ Unadhani ni nani? Nd’o huyuhuyu choko
aliyetuibia... Kwani nani mwingine.’’ Sauti nyingine ilisikika ikikoroma. Mara
ngumi moja ya kichwa ikatua mwilini mwa Maduhu, maumivu yakaandamana na kilio
cha nguvu kutoka kwake. Hajakaa sawa, mara akapokea kofi la uso, kutoka katika
mkono uliyoshiba kimazoezi. Akiwa katika sintofahau, mara akahisi kama harufu
fulani ya damu. Pakepale pua zake mbili zikaanza kutoa damu. Hakupata muda wa
kuuliza ama kujiuliza ni kipi alichokosea hadi kipigo kimuangukie?
ENDELEA... Mtoto yule
mwene umri wa miaka saba pekee. Aliinamisha kichwa chake chini na kuruhusu damu
kutoka puani imwagike, huku akisahau kuwa wale watu waliyokuwa wamemzunguka
hawakuwa wameishia hapo. Akiwa kainamisha kichwa mara kofi jingine likatua
katika uso wake kwa mara nyingine pasina kuhofia damu zilizokuwa zikimtoka
mtoto yule. Hapo maumivu yakamzidi, akawaza nini afanye? Na vipi anakutana na
kipigo namna ile utadhani ameikosea dunia. Wakati akijiuliza, mara ikasikika
sauti ya kike.
‘’ Jamani, ni
bora tumpeleke moja kwa moja kituoni huyu mtoto, itakuwaje atuibie pesa zote za
sherehe?’’ Ha! Hapo mwili mzima wa mtoto yule ukamsisimka, hofu ikamjaa huku
akiwaza jambo lile jipya alilofikishiwa, ati kapora pesa za sherehe! Saa ngapi?
Hata hivyo, makelele ya waliyomzunguka hayakuweza kumpatia hata muda wa
kujiwazia. Ni wazi, waliyomzunguka walikuwa na hasira sana, mmoja kati yao
alimbebelea kwa mikono miwili na bila huruma akamtupa kwa nguvu chini na
kumsababishia mtoto yule atoe ukelele mkali. Kisha wakamchukuwa mzobemzobe na
safari ya kuanza kumpeleka kituoni ikaanza.
Wakati huo, hakuna
ambaye hakutaka kuamini kuwa mtoto yule si mwizi. Kila mmoja aliamini kuwa,
hakuna aliyeiba isipokuwa yeye maana hata wakati pesa zile zinaibiwa, mwizi
alikuwa amevalia mavazi machafu ya kichokoraa kama yeye huku hata umri wakiwa
wanaendana. Hatimae walimfikisha kituoni.
Huko
kituoni pia hakukuwa na msalie mtume. Kipigo cha mbwa mwizi kilimwangukia kama
hana akili vizuri huku aking’ang’anizwa aweze kukili kuiba pesa zile ambazo
hata hazifahamu na wala hafahamu ninani aliyeziiba. Adhabu mbalimbali alipatiwa
tena bila kuhurumiwa, alipokili kuumizwa na adhabu zile, waadhibu hawakumwacha
waliendelea kumuadhibu haswa! Huku wakimlazimisha akubali kuwa, yeye nd’o mtu
aliyeziiba pesa zile.
Ingawa
alikuwa mtoto mdogo lakini hakuwa mjinga kiasi cha kukubali jambo lisilomuhusu.
Adhabu zilimpelekea kupoteza hadi fahamu,
akawa hajitambui na wala hatambui kilichokuwa kikiendelea.
Muda wote huo wa adhabu, wale waliyomleta
tayari walikuwa wameshaondoka zamani sana. Lakini baada ya muda kupita
walirejea kwa mara nyingine kituoni huku wakiwa na mtoto mwingine aliyevalia
kama yeye.
‘’ Afande, tunaomba mtuwie radhi... Huyo mtoto
aliyemo ndani hana hatia, mwenye hatia ni huyu hapa.’’ Mwanaume mmoja
aliyeonekana na sura ya ghadhabu alisema maneno yale.
‘’ Kwahiyo, mnataka kusema yule hahusiki na
lolote? Mbona amekaa kama kibaka tu?’’
‘’ Ndivyo afande. Mwizi ni huyu hapa,
tumembamba sehemu, yule mtoto tulimfananiha tu.’’ Bwana mwingine alisema huku
yeye akiongeza kwa kumpiga makone kadhaa mtoto ambaye walikuwa wameshikilia.
Kituoni hakuna maswala ya kuuliza,
walimchukuwa mtoto mwingine aliyeletwa pale ambaye kiasi fulani yeye alionekana
kuwa nunda maana alijaribu hadi kuwabishia wao. Hapo afande mmoja akaamua
kumuonesha kazi ya rungu. Mtoto yule hakukubali kuyastahimili maumivu
aliyoyapata, kwa hasira akajibu mashambulizi kwa kumrushia kichwa afande
aliyehusika kumpiga rungu lile. Akawa amechokoza nyoka bila mweyewe kujitambua.
Hapo ndipo alipokipata cha mtema kuni.
Maduhu alipozinduka alishangaa sana baada ya
kuona hajafungwa pingu mikononi na wala hayupo ndani ya kile chumb cha
mateso. Hata baada ya kuonduka, wale
waliyomleta kituoni walichukuwa jukumu la kweda kumtibisha huku wakimwomba
msamaha.
Alikaa hospitali kwa muda wa siku tatu
kutokana na majiraha aliyokuwanayo. Kuna wakati alikuwa akikumbuka mbali sana,
kipindicha nyuma.
***
‘’
Mdogo wangu, najua unajuawazi kuwa, maisha yetu ni magumu na hiyo ni sababu
hata ya sisi kutokusoma, ila usijali... Mimi nitatafuta pesa kuhakikisha wewe
siku moja unaingia darasani.’’
‘’ Nimekuelewa kaka. Lakini, kwanini sisi
tunasemwa vibaya, iwe nyumbani? Iwe shuleni.’’
‘’ Ni kwasababu sisi hatuna pesa. Ila ipo
siku watatuheshimu tu... Futa machozi mdogo wangu.’’
***
Kumbukumbu zile ziliambatana na kilio. Hakutaka
kuamini kama wazazi wake pamoja na kaka yake hawapo tena ndani ya dunia hiyo.
Akifikiria ni wapi ataelekea? Ni kweli kabisa, historia ya baba yake haikuwa na
mantiki sana. Inasemekana kuwa, baada ya kuhamia ndani ya jiji hilo ambalo
kwalo ndiko alianza maisha mapya, alitoka katika mji mmoja ambao upo mkoa wa
mbali sana na jiji hilo, hakuhitaji tena kurejea nyumbani kwao ingawa
hakikujulikana kisa cha yeye kutokuhitaji kurejea huko. Hata alipofika katika
jiji hilo alilofia, alikutana na mwanamke mmoja ambaye naye pia ni marehemu;
mama yule alikuwa akifanya kazi za ndani huku maisha yake pia yakiwa hayana
mbele wala nyuma. Wakapendana, mpenzi yao yakafika mbali zaidi hadi wkajikuta
kwa bahati mbaya mimba inamuingia mwanamke yule. Hapo ikawa kasheshe. Akatimuliwa
kule alipokuwa akifanyia kazi, ndipo hapo alipoanza kuishi rasimi na manaume
yule. Ingawa mwanzoni maisha yao yalikuwa ya kawaida lakini kuzaliwa kwa watoto
kidogo kulikuja na mabalaa. Kipato kikashuka wakashindwa hata kuwa wakijikimu,
wimbi la umasikini likawavaa haswahaswa bila utani.
Nguo wakawa wakivaliana, baba akiwarithisha
hadi wanae nguo zake. Mawazo mengi sana kuhusu familia, yalimpelekea mzee yule
akijikute akikumbwa na ugonjwa usiyojulikana. Na huo nd’o ugonjwa ulliyomtwaa.
Huku akionmdoka na roho ya mkewe pamoja na ,mwanae, wakamwacha mtoto mogo
mwenye umri wa miaka saba. Asiyejua mbele wai wala nyuma wapi.
Mtoto yule yatima, tayari mateso ya kuwa
mbali na wazazi yalianza kumpata. Akaanza kugundua kumbe ukiwa yatima
huthaminiwi, ukiwa fukara huangaliwi. Watui wapo radhi wakuondoe hata kwenye
ulimwengu. Akiwa bado katika tafakari nzito huku bado ruhusa kutoka kwa daktari
haijamfika. Alijikuta akipandwa na uchungu.
‘’ Wazazi wangu... Kwanini lakini
mmeondoka? Kwanini mmeniacha katika mateso haya? Tazama, simtambui ndugu yeyote
kutoka kwa baba wala kwa mama. Ni vipi nitaweza kuishi ndani ya dunia hii?
Dunia isiyenithamini wala isiyo nihurumia? Wazazi, ikiwa ninyi ndio tegemeo
langu kuu na mmeniacha, mnadhani nitakuwaje? Ona, ninateswa bila hata kosa...’’
Alilalamika sana, lakini hakuna kilichobadilika, zaidi ni badliko la sura
pekee. Uso ukitengeneza tabasamu la kununa huku machozi yakimmiminika.
Muda kidogo, daktari aliingia ndani mule na
kumwita nmtoto yule hospitali kisha akamweleza kuwa, angependa kumruhusu aweze
kwenda maana tayari hali yake ilikuwa nzuri.
‘’ Dokta, samahani sana... Wewe ni kama baba
yangu, na ninaimani unawatoto kama mimi. Tafadhali naomba uniachie niendelee
walau kuishi hapahapa hospitali, huko nje sipawezi mimi. Wazazi wangu
wamefariki, sijui hata wapi nielekee. Sina ndugu wala jamaa yeyote katika hii
dunia.’’ Mtoto yule aliongea hayo kwa uchungu baada ya kuwa amepewa ruhusa ya
kuondoka hospitali pale.
Daktari akamtazama mtoto yule kwa jicho la huruma
utadhani mtu mwenye kuhitaji kumsaidia kisha akasema,
‘’Hospitali
ni sehemu ya wagonjwa tu na si watu wazima. Hata hivyo, unaonekana kijana mdogo
sana ambaye bado matatizo hujayazoea. Ni watoto wengi na hata wakubwa wenye
matatizo tena zaidi yako wanakuja hapa na kuomba kama unavyoomba wewe, lakini
tunashindwa jinsi ya kuwasaidia. Labda nikusaidie kwa kusema. Mwanaume wa kweli
huwa hayaogopi matatizo, nenda hukohuko yalipo ili uweze kukuwa ki akili na
kutengemaa kifikra, sisi pia tumepitia magumu, na kupitia hayo tumejifunza na
kuwa hapa tulipo leo.’’
ITAENDELEA.
0 comments:
Post a Comment