IMELETWA KWAKO NA: SIMULIZIMIX ENTERTAINMENT.
MWANDISHI: FRANK MASAI.
UTANGULIZI.
Ni katika nchi ya Tanzania nchi inayo aminika kua na utajiri
mkubwa sana ingawaje asilimia kubwa ya wananchi wake ni masikini, kuna sehemu
mwandishi anauliza inawezekanaje wananchi wakawa matajiri wakati wengi wa
viongozi wanajali matumbo yao kwanza ambayo hata hayajai…. Na ni ndani ya nchi
hiyo hiyo inayosemekana ni nchi ya kidemocrasia lakini bado mwandishi akauliza
utasemaje ni nchi ya democrasia wakati ukitaka kusema unazimwa, wala mwandishi
hakutaka kuyazungumzia hayo katika simulizi hii alichosema ni kua embu taachane
na hayo maana haya husiki katika simulizi hii ila yanayo husika katika simulizi
hii ni haya.
DUKA LA ROHO ni kikosi kinachoendesha matendo ya kigaidi
ndani ya nchi ya Tanzania huku wakidai kua kazi yao kubwa ni kuuza na kununua
roho za watu… Yani kama ukiingilia mipango yao basi unakua umeiweka roho yako
au roho za uwapendao dukani ambapo itakubidi uinunue roho yako au roho za
uwapendao kwa kufanya kile watakacho kitaka wao au uuze roho yako au za
uwapendao kwa kutotii kile walicho kutaka wewe ukifanye.. kwa kufanya hivyo viongozi wengi ambao
wanafanya kazi kwa kufuata sharia wanaondolewa duniani na wengine wanalazimishwa
kujiuzuru kutoka katika nyazifa mbali mbali ili kuzinunua roho zao au za
wawapendao baada ya kua zimewekwa dukani na kikosi hiki cha duka la roho.
Mbaya Zaidi ni kua raisi wa nchi hiyo ya Tanzania nae roho
yake imewekwa dukani hivyo anaendeshwa na kikundi hicho cha DUKA LA ROHO jambo
linalomfanya afanye maamuzi ya ajabu yanayoshangaza wananchi wake ikiwemo
kuwafukuza kazi viongozi na wanausalama wanaofanya kazi kwa kufata haki na
sharia ya nchi na kuwateua viongozi na wanausalama ambao ni vibaraka wa DUKA LA
ROHO ambao wanafanya kazi kwa kufata matakwa ya kikosi hicho na si haki ya
wananchi.
Lakini anakuepo kijana mmoja ambae ni mtanzania halisi mwenye uwezo mkubwa wa kupigana iwe ni kwa
kutumia siraha au mapigano ya ana kwa ana basi ukiingia katika anga za huyo
kijana basi hutoki…. Kubwa kuliko yote ni uwezo wake mkubwa katika mambo ya
sayansi na technolojia…. Aliwahi kusomea chuo cha sayansi nchini china na akawa
ni moja kati ya wanasayansi sita walio wahi kutengeneza mtambo mmoja uitwao SGT
wenye uwezo mkubwa sana duniani na wenye uwezo wa kufanya kazi nyingi sana za
kipelelezi…. Ikiwemo uwezo wa kuzima satellite zote duniani na aina zote za
mawasiliano na kuweza kuiba siri za nchi za nchi yoyote
Wakati kikundi hiki cha duka la roho kinashamili kuendesha
matendo ya kigaidi nchini Tanzania kijana huyu alikua mafichoni nchi za mbali
hii ni kutokana na kua anatafutwa sana na afisa usalama wa Tanzania tu, bali
pia anatafutwa vikali na shirika la kipelelezi la marekani FBI hii ni kutokana
na matukio makubwa aliyowahi kuyafanya huko nyuma kwa kutumia uwezo wake wa
kisayansi ikiwepo kuiba kwa kutumia technologia…. FBI wanamtafta sana
wanashindwa kumpata yote hayo ni kwa sababu ya uwezo wake wa kucheza na
technoloji kwa kuzuia aina yoyote ya vifaa vya kipelelezi vinavyoweza kung’amua
ni wapi alipo.
Baada ya maovu ya kikudi cha DUKA LA ROHO kuzidi mbaya Zaidi
kufikia sehemu ambayo wanaiweka dukani roho ya mtoto wa kijana huyo ambaye ndo
yuko mafichoni nchi za mbali kwa kumpa masaa 24 mama wa mtoto huyo ambae ni
mwanamke aliyezaa na kijana huyo kuweza kujipeleka mwenyewe mikononi mwa kikundi hicho ili kuweza kununua
roho ya mwanae kwa kuiuza roho yake. Na hii ni baada ya kwenda kinyume na mipango
ya kikosi hicho cha duka la roho… Lakini kijana yule alie mafichoni anapata
kunasa mpango mzima wa kikosi hicho hivyo anafunga safari kutoka huko mafichoni
kwa lengo moja tu kuja kuiokoa familia yake.
Anafanikiwa kuzuia mpango wa kikosi cha DUKA LA ROHO wa
kuiteketeza familia yake lakini pia anafanikiwa kuzuia mashambulizi mengi ya
kigaidi yaliyokua yamepangwa kufanywa na kikosi hicho ndani ya nchi ya Tanzania yote hayo anayafanya
kwa kutumia uwezo wake mkubwa wa kucheza na sayansi na technolojia lakini pia
kwa uwezo wake wa mapigano ya ana kwa ana.
Kwa kutambau uwezo wa kijana huyo kikosi cha Duka la roho
kinatafuta kila njia ya kumuangamiza wanashindwa…. Mpaka wanatumwa wauwaji wa
kimataifa wa kizungu “Pro killers” ambao hawajawahi shindwa mission yoyote na wameuwa watu wengi sana ili kwa mikono ya
kijana huyo wanajikuta wakiuliwa wao… Hapo ndo kikundi cha DUKA LA ROHO kinaona
njia pekee ya kumnasa kijana huyo ni kuishinikiza serekali iweze kumtafuta na
kumkabizisha kwao ila kiukweli hata serikali yenyewe haina jinsi ya kumkamata
kijana huyo… Kikundi hicho bila kujali kua hata serikali haiwezi kumkamata
kijana huyo chenyewe kinaanza kuendesha mauaji ya askari popote askari atakapoonekana
wenyewe ni wanaua wakidai mauaji hayo yatakoma mara tu serikali itakapo
wakabidhi kijana huyo…
Baada ya mauaji ya askari kuzidi kijana huyo anawasiliana na
raisi wa nchi na raisi kwa kutambua uwezo wa kijana huyo anamuomba kijana huyo
waungane ili kuweza kuteketeza kikosi hicho cha DUKA LA ROHO ingawa rahisi
anajua fika kijana huyo anatafutwa kila kona sio na Tanzania tu bali pia na shirika la
kipelelezi la marekani FBI. Makubaliano yanapitishwa na raisi anamkabidhi
kijana huyo siraha zote alizo zihitaji kwa lengo la kuteketeza kabisa kikundi
cha duka la roho.
Kijana huyo akiwa na kikosi kidogo cha wanausalama ambao
walifukuzwa kazi na raisi baada ya kuanza kufatilia kikundi hicho cha DUKA LA
ROHO..... Je wataweza kufanikiwa kukiteketeza kikosi hicho?
UNAWEZAJE SASA KUKOSA KUFATILIA HADITHI HII NZURI YA
MAPIGANO? HADITHI ILIYOPANGILIWA MATUKIO NA MWANDISHI WETU KWA JINSI AMBAYO
ITAWEZA KUKUBURUDISHA, KUKUSISIMUA NA KUKUELIMISHA… HIVYO USIKOSE KUFATILIA
HADITHI HII KUJUA KIJANA HUYO WA KITANZANIA MWENYE UWEZO MKUBWA WA KISAYANSI,
MAPIGANO YA KIVITA NA MAPIGANO YA ANA KWA ANA, NI NANI? NA NI YAPI MAKUBWA YA
KUFURAHISHA NA KUSHANGAZA ALIYOYAFANYA NDANI YA SIMULIZI HII… HAKIKA UTAFURAHI
NA KUBURUDIKA KWA KAZI ZAKE MWANANA ALIZO ZIFANYA NDANI YA HADITHI HII…. PIA UTAWEZA KUJUA NI WATU GANI WANAOKIENDESHA
KIKOSI HICHO CHA DUKA LA ROHO PIA UTATAMBUA UWEZO WAO WA KUTISHA KATIKA
KUZIFANYA KAZI ZAO JAPO PAMOJA NA UWEZO WAO HAWAKUWEZA KUPITA KATIKA MIKONO YA
KIJANA WETU MASHUHULI.. USIKOSE NA UNGANA NA SIMULIZI MIX ENTERTAINMENT AMBAO WATAKULETEA KISA HIKI MWANZO MPAKA MWISHO… SALUTI KWA FRANK MASAI AMBAE YEYE NDO MTUNZI NA
MWANDISHI WA HADITHI HII. JAMAA MMOJA ANAFANYA KAZI ZAKE VIZURI SANA NA UTAUSOMA UWEZO WAKE KUPITIA HADITHI HII
KUSOMA SEHEMU YA KWANZA BOFYA HAPA DUKA LA ROHO 01
UTAPATA HADITHI HII NA NYINGINE NYINGI ZITAKAZOLETWA KWAKO NA SIMULIZI MIX ENTERTAINMENT KATIKA BLOG www.simulizimix.com FACEBOOK, INTAGRAM NA TWITTER @simulizimix .. YOUTUBE Simulizi Mix Entertainment WHATSAPP 0712505163 ... TUMA NENO GROUP KUONGEZWA KWENYE MAGRUP YA SIMULIZI MIX ENTERTAINMENT AU TUMA NENO INBOX KUPATA SIMULIZI ZETU INBOX YA SIMU YAKO., UKITUMA NENO INBOX HAKIKISHA UMASAVE NAMBA YETU KWENYE SIMU YAKO.
SHARING IS CARING, USISAHAU KUCOMENT LAKINI PIA KUSHARE HADITHI ZETU KWAUWAPENDAO NDUGU JAMAA NA MARAFIKI ILI UWEZE KUBURUDIKA NA KUELIMIKA PAMOJA NAO.
SIMULIZI MIX ENTERTAINMENT WE TOUCH YOUR FEELINGS
0 comments:
Post a Comment