IMELETWA KWAKO NA SIMULIZ MIX ENTERTAINMENT
MWANDISHI NI FRANK MASAI
SEHEMU YA PILI
ILIPOISHIA
"Ooooh! Ni Prince
Mubarak." Jamaa yule aliongea baada ya kujifuta damu zilizokuwa
zinamchuruzika. "Na swali.moja tu kwako, na usipolijibu, nitakupa onyo
tu." Jamaa alimtazama Mubah kabla hajauliza swali lake. "Kwa nini
umeamua kuweka dukani roho za uwapendao?" Jamaa alimuuliza Mubah lakini
badala ya Mubah kujibu, yeye akachukua gundi aina ya 'sole tape' na kuizungusha
mdomoni mwa mtuhumiwa yule mwenye mdomo wa kero na kukereketa.
"Thats will help, I
think. (Hiyo itasaidia nadhani)" Lisa aliongea akikubaliana na kitendo
kilichofanywa na Mubah.
ENDELEA
**** Safari yao ilikomea eneo moja la ufukwe
wa bahari ya hindi. Na baada ya hapo, Lisa alitoa simu yake ya mkononi na
kuipiga. Maongezi yalichukua dakika
chache na simu ikakatwa.
Baada ya dakika
zisizozidi kumi za kukata simu ile, kwa mbali, kwa kutumia darubini yake, Lisa
aliona Nyambizi ikiibuka toka chini ya bahari na baadae ikafunguka kwa juu na
boti ndogo saba zikatoka ndani yake. Boti hizo ni zile ziwezazo kubeba watu
wawili kila boti moja. Waendeshaji
walikuwa wamevalia mavazi ya kuogolea na bunduki aina M16 zikiwa migongoni mwao.
Lisa akashushia darubini yake kifuani na kuwapa ishara wenzake ya kujiandaa
hasa kutoka mle garini.
Boti saba zikasimama
mbele ya wakubwa wa kazi, na kitendo bila kuchelewa, kundi linaloongozwa na
Lisa likiwa na mtuhumiwa wao, wakakwea nyuma ya boti hizo ndogo na safari fupi
ya kwenda kwenye Nyambizi moja ndogo kiasi, ikaanza.
Boti tano zikiwa mbele na
nyingine mbili nyuma zikilinda usalama ili yule mtuhumiwa asitoroke, zikazidi
kukata maji kuelekea kwenye nyambizi. Wakiwa katika umbali fulani, Lisa
alimuamuru dereva wa boti yake asimame. Naye baada ya kusimama, Lisa aligeuka
nyuma na kuangalia kule alipotoka.
Kulikuwa hakuna watu
wanaozunguka eneo lile, hiyo ikawa nafasi pekee ya Lisa kufanya alichokusudia.
Akatoa rimoti ndogo
ambayo alibofya kitufe kimoja kilichokuwepo katikati. Na hapohapo, mlipuko
mkubwa uliikumba ardhi ambayo gari aina ya Noah ilikuwa imeweka makao kwa
muda. Ni ile gari ambayo walikuwa
wanaitumia Lisa na kundi lake. Baada ya kumalizia kazi ambayo waliipanga, sasa
waliiteketeza na kuacha Jiji dogo la Dar Es Salaam kutetemeka kwa huo mlipuko.
Wafanyakazi wa maeneo yale walikimbia huku na huko wakihisi jiji limevamiwa na
magaidi hatari. Hakuna aliyekumbuka kugeuka nyuma, wote walikuwa wakinusuru
roho zao. Hakika ilikuwa ni mshike mshike maeneo yale.
Baada ya kulidhika na kazi
yake, Lisa akamgonga bega kumruhusu dereva wake aondoke, naye akatii amri na
kwenda sehemu ambayo walipanga waende. **** Ndani ya nyambizi ile, kulikuwa
kuna pilika za hapa na pale hasa wale mafundi mitambo wanaongoza chombo kile
maalumu kwa ajili ya kazi za kijeshi au kiusalama. Naam, baada ya Lisa na kundi
lake wakiwa sambamba na mtuhumiwa wao kuingia kwenye chombo kile, waliongozwa
kwenye chumba maalumu na kuoneshwa nafasi zao za kukaa. Baada ya kukaa, alitokea daktari mmoja
akiongozana na kijana aliyebeba sinia dogo lililokuwa na sindano uwezazo
kuzikamata kama bastola. Sindano hizo zenye dawa kiasi, kila mmoja alichomwa
begani na baada ya dakika chache, macho ya hawa watu yakaanza kuwa mazito.
"Kazi za utumwa
hizi. Hamtakiwi kujua hata ni wapi mnafanyia kazi na ndio maana mnapigwa
sindano za usingizi ili msione mnapoenda. Stupid peoples." Sauti nzito
iliyochanganyanyika na ulevi, ilimtoka yule mtuhumiwa aliyekuwa huru kuongea
baada ya kutolewa ile gundi aliyozungushiwa na Mubah. Hakuna aliyemjibu na
badala yake, kila mmoja alibebwa na usingizi mzito. ****
FISSA (Federal
Intelligence Secret Service Agencies)
Mlango mmoja mkubwa
uliandikwa maandishi hayo ambapo ndipo hasa Lisa na Mubah wanafanya kazi zao.
Ule usingizi mrefu ulikuwa umewapaa na sasa walikuwa wanatembea wenyewe huku
wakimkwida vema mtuhumiwa wao ili asiwaponyoke.
"Kazi nzuri Agent
Lisa. Mmefanya vizuri na kikosi chako." Sauti ya mtu mmoja mrefu kiasi na
mweusi, ilisikika ikiwa kwenye jukwaa dogo ambalo mbele yake kulikuwa na watu
wanachakalika na kompyuta zao huku skrini moja kubwa ikionesha kazi nzima
wafanyazo wale wafanyakazi.
"Asante mkuu."
Lisa alishukuru huku akiinama kidogo kuonesha heshima kwa mkuu wake wa kazi.
Mkuu yule akashuka toka kwenye lile jukwaa na moja kwa moja akamfuata yule
mtuhumiwa na kumuangalia kwa macho makali kabla hajaanza kuongea.
"John Lobo.
Nilishangaa sana nilipoambiwa kuwa u mzima. Nilikuua kwa mikono yangu, lakini
leo ni kama nakutana na mzimu." Sauti ya yule bwana ilipenyeza kwenye
masikio ya kila mmoja aliyesikia vema maongezi yale. "Sina kesi na wewe.
Nilishakuua kipindi kile, hapa naanza na kesi nyingine." Alimaliza Mkuu wa
FISSA na kugeuka nyuma kurudi kwenye lile jukwaa dogo.
"Malocha
Malingumu." Sauti ya John Lobo, mtuhumiwa aliyekamatwa na kundi la Lisa,
ilimuita yule mkuu wa kitengo cha siri cha huduma za kipelelezi nchini
Tanzania. Bwana Malocha akasimama kumsikiliza kimtokacho John Lobo. "Siyo
kosa langu kuua familia yako. Nilinunua roho zao kwa kuamrishwa na shetani
langu. Usilalamike sana. Hahahahahaaa." Lobo alimaliza kwa cheko lake la
kukera kushinda hata la katuni au fisi.
"Mpelekeni Hell in
Hell." Malocha akaamuru na kila mmoja alishituka baada ya kusikia amri
hiyo. "Hamjanisikia?" Malocha aliuliza baada ya kuona hakuna
kinachotendeka baada ya amri.
"Lakini Mkuu huyu
tutampoteza kule. Kumbuka CIA na FBi wanamtaka mzima." Lisa akiongea
kumuelewesha mkuu wake.
"Kwa hiyo unashauri
apelekwe wapi?" Malocha akauliza tena swali.
"Nadhani twende naye
123K." Alitoa wazo Lisa.
"Kwa hiyo akakae tu!
Kaja kukaa hapa au kusema ukweli?" Malocha alimtupia swali Lisa.
"Lakini si kumpeleka
Hell in Hell. Atasema nini kule?" Lisa alijitetea.
"Hivi mmenileta huku
nije kusema kitu au nije kupiga story na 'school mate' wenzangu?" Lobo
alifungua kinywa chake na kuwauliza wale wanaoshauriana wapi wampeleke.
"Kama mnataka mnijue au niseme chochote, hilo mmekosea. Hapa hampati kitu
wajinga nyie." Lobo akamaliza na hapohapo ngumi nzito ya tumbo ilitua.
Alikuwa ni Mubah aliyemuadabisha.
"Utalipa hii
dogo." Lobo alimwambia Mubah na Mubah badala ya kutilia maanani yale
maneno, alimuongeza konde lingine zito la tumboni.
"Big Mistake(Kosa
kubwa) Lakini bado unanafasi ya kulisawazisha." Lobo alimwambia tena Mubah
baada ya kuinuka alipokuwa kainama kwa sababu ya kupigwa ngumi ile.
"Mpelekeni
123F6."Malocha aliamuru tena. Na kitendo bila kuchelewa, Lisa na Mubarak
walimkamata kushoto na kulia na kuanza kumkokota kwenda chumba walichokiita
123F6.
HELL IN HELL
Hichi ni chumba kipana
kilichopo ndani ya FISSA. Ndani ya chumba hiki kuna kiti cha umeme ambacho
hutumika kuwasulubu watuhumiwa nguri na saa nyingine kuwaua.
Pia kuna tank kubwa
ambalo limejengwa kwa vioo, na tank hilo ndani yake kuna maji. Pia hutumika
kusulubisha watuhumiwa kwa kuwazamisha humo au wakiona haongei, hufungulia
umeme uliyoungwa ndani ya tank hilo na kuanza kumpiga shoti mtuhumiwa. Hizo ni
silaha chache zilizopo katika chumba kiitwacho Hell In Hell. Mbali na hayo,
kuna vifaa vya kunyongea na kuchania ngozi.
Ni chumba ambacho kinaogopwa hata na wafanyakazi wenyewe. Kinatisha kwa
matendo yanayofanyika huko.
123K
Hiki pia ni chumba
kilichopo hukohuko FISSA. Chumba hiki pia ni kipana na kina meza moja kubwa
pamoja na kioo ambacho ukiwa ndani huwezi kumuona wa nje lakini wa nje anamuona
wa ndani. Chumba hichi ni kwa ajili ya kumuhoji mtuhumiwa kwa mdomo bila
kumsulubisha. Na hata kama watataka.kufanya hivyo, basi hutumia viungo vyao
kama ngumi na mateke.
123F6
Hiki ni chumba kipana pia
kwa ajili ya mahojiano na watuhumiwa. Ndani ya chumba hiki, mahojiano huwa ni ya
kulazimisha uongee ukweli kwa kubanwa na silaha mbalimbali pamoja kuchomwa na
vitu vyenye ncha kali lakini lengo likiwa utoke mzima. Na mara nyingi kama mtuhumiwa ni mgumu, basi
hupigwa sindano yenye dawa kali ambayo hufanya ubongo na akili ya mtuhumiwa
iwaze kusema ukweli tu.
Humo ndimo ambamo John
Lobo kapelekwa. Nyuso mbili ambazo hazina utani zilikuwa zimesimama pembeni ya
chumba hicho huku wakijaribu jaribu vifaa vyao. Mzee mmoja ambaye alikuwa
anapuliza gesi yenye moto juu, aligeuka haraka baada ya kusikia mlango wa
chumba kile ukifunguliwa.
"Ooh! Lisa.
Umefanikiwa kumkamata Lobo. Kazi nzuri sana binti." Mzee yule aliongea
kumpongeza Lisa.
"Asante Babu Pujini,
hakuleta shida wakati wa kumkamata." Lisa alimjibu Mzee Pujini ambaye
alikuwa ana asili fulani ya Kihindi lakini ni Muafrika halisi kutoka Tanzania.
"Good Lisa. Ndio
umemleta kwenye shughuli eeh." Mzee Pujini aliongea huku akianza kuchezea
tena ile gesi kwenye kibubu maalumu kinachotengeneza moto huo wa gesi.
"Ndio babu. Fanya
yako." Lisa alijibu na wakati huo Mubah alikuwa anafungua pingu alizokuwa
kamfunga John Lobo.
Licha ya Lisa na Mzee
Pujini kuongea mengi yanayomhusu John Lobo, lakini Lobo mwenyewe hakuwepo
kwenye dunia yao bali macho yake yalikuwa yakipepesa huku na huko, chini na juu
ya chumba kile.
"Huyu hapa
Mzee." Sauti ya Mubarak ilisikika huku ikifuatiwa na kumsukuma Lobo kwa
mzee yule bingwa wa kutoa adhabu kwa watuhumiwa mbalimbali.
"Beda. Muondoe
misuti yake huyu bwana." Mzee Pujini alimsukumia Lobo kwa Beda, jamaa
fulani wa makamo na kwenye mwili mkubwa kutokana na kunyanyua vitu vizito.
Naye Beda bila kuchelewa,
akaanza kumwondoa nguo John Lobo na wakati huo Lisa na Mubah walishatoka katika
chumba kile na Mzee Pujini alishakifunga.
ITAENDELEA
JE NI MATESO GANI ALIYAPATA KIJANA ROBO? BOFYA HAPA>> SEHEMU YA TATU KUJUA NI NINI KILITOKEA
0 comments:
Post a Comment