Tuesday, June 20, 2017

IMELETWA KWAKO NA SIMULIZI MIX ENTERTAINMENT
MWANDISHI: FRANK MASAI
SEHEMU YA TATU

ILIPOISHIA 
"Beda. Muondoe misuti yake huyu bwana." Mzee Pujini alimsukumia Lobo kwa Beda, jamaa fulani wa makamo na kwenye mwili mkubwa kutokana na kunyanyua vitu vizito.
Naye Beda bila kuchelewa, akaanza kumwondoa nguo John Lobo na wakati huo Lisa na Mubah walishatoka katika chumba kile na Mzee Pujini alishakifunga. 

ENDELEA 
****
"Lobo. Nia yako na washirika wako ni nini?" Sauti ya kiume ilisikika katika chumba kiitwacho 123F6.  Ilikuwa ni sauti ya Malocha ikitoka kwenye spika zilizopo kwenye chumba kile.
Lobo alikuwa akivuja damu nyingi kifuani na maeneo ya usoni. Alikuwa kalegea kwa mateso makali ambayo yalitoka mikononi mwa Beda na Mzee Pujini.
"Kazi yangu ni kuuza au kununua roho tu! Sina kazi nyingine. Sina nia na wala sijui washirika wangu ni wakina nani." Lobo alijibu swali la Malocha na baada ya jibu hilo, Malocha alitoa ruhusa ya mateso kuendelea.
Mzee Pujini akachukua kile kibubu chenye gesi na kuwasha gesi ile. Baada ya kuweka moto fulani kwenye kibubu kile cha gesi, akamfata Lobo na kuanza kumpitishia machoni bila kumdhuru bali kumsikilizisha joto litokalo mle kwenye kibubu.
"Joto hili linaenda kwenye maungo yako ya uzazi." Mzee Pujini akiwa kavalia kama Daktari, akaongea huku taratibu akianza kushusha moto ule kwenye maeneo ambayo kayataja.
Licha ya hayo yote kutukia, uso wa John Lobo ulikuwa si wenye mashaka wala uoga. Ni kama alishazoea yale mateso, lakini yote ni sababu alikuwa mkomavu katika nyanja kama zile.
Mzee Pujini akafika maeneo ya uzazi ya John Lobo, na bila kusita akapulizia gesi ya moto maeneo yale na kumfanya John Lobo atoe sauti kali iliyochanganyika na maumivu. Hakika mkomavu na kamanda wa mateso, alikuwa anaumia.
"You fu**n, motherfu***r you're hurting me. (We mpumbavu, (tusi). Unaniumiza)." Sauti ya maumivu makali ilisikika kutoka kwenye kinywa cha Lobo ikifuatana na matusi mazito ya wazazi kumuelekea Mzee Pujini.
"Sema ukweli tuache hili zoezi." Mzee Pujini aliacha kuchoka maeneo nyeti ya Lobo na kumuomba aseme ukweli.
"Pale nitakapofanikiwa kusimama kwenye hiki kiti, wewe ndio utakuwa wa kwanza kufa." John Lobo alimwambia Mzee Pujini maneno ambayo yule mzee alitabasamu kwa dharau kisha akaangalia kile kioo ambacho wa ndani hamuoni wa nje ikiwa ni ishara ya kuwaambia waulize swali lingine.
"Lobo. Hatupo hapa kukuumiza. Ni rahisi tu! Unashirikiana na nani na nini nia yako kwa ufanyayo." Swali lilelile lilitoka kwenye kinywa cha Malocha.
"Hahahaaa. Malocha, mbona unajiumiza sana. Nimekwisha kwambia, sina nia zaidi ya kuuza na kununua roho za watu. Au unataka nikwambie duka la roho lilipo?" Lobo aliuliza huku uso wake ukielekea kwenye kile kioo kana kwamba anawaona wale wanaomtupia maswali kwa kunong'onezana.
"Lobo. Hatupo katika utani. Umemuua Kamanda wa Kikosi cha Upepelezi kanda ya kati. Umewatishia amani mawaziri mbalimbali na kauli yako ya kununua roho zao. Ukawaua baadhi ya viongozi hao. Ukaona haitoshi, ukaanza kuwaondoa mabalozi mbalimbali wa nchi hii kwa kuwaua. Sasa umegusa pabaya zaidi. Marekani. Umegusa nchi ambayo hatuiwezi kwa kitu chochote....." Sauti ya Malocha ilikuwa ikielezea baadhi ya maovu ya John Lobo lakini kabla hajamaliza maongezi yake, sauti yenye hasira kupindukia, ilimkata kauli.
"Eti hatuiwezi kwa chochote. Ni ujinga gani ambao umekujaa kichwani we' mpumbavu? Marekani anachotuweza ni nini? Au ndio kasumba zenu za uoga bado zimewatawala kichwani mwenu?  Huyu Frank anapambana na kutafutwa kwa udi na uvumba na watu gani? Si ni hawahawa Wamarekani? Mbona hawampati? Mbona hata wakimpata wanamshindwa? Kaua makomando wangapi Wakimarekani. Usiwe mjinga Malocha. Umiza kichwa fala wewe." Kauli chafu zilitiririka toka kinywani mwa Lobo na hakuna aliyethubutu kumkatiza hadi alipomaliza mwenyewe.
"Sound like it's true. But none of it is real. (Sauti kama ya ukweli. Lakini hakuna kati hivyo chenye uhalisia)." Malocha aliongea kwa kutumia lugha ya ughaibuni. "Frank, never killed any commander from America. He just killed the terrorists, and bad guys. (Frank hakuua kamanda yeyote wa Kimarekani. Aliua wavamizi na watu wabaya pekee)." Sauti ya Lisa iliunga maelezo ambayo Malocha aliyaacha kati.
"Inaonekana hamjui lolote la kwa nini Frank anatafutwa na kwa nini kajificha. Na mbaya zaidi, hao anaowaua ndio mimi na baadhi yenu nyie wapelelezi mnawasujudia. Mtakufa kama panya kwenye sumu kwa mkono wangu." Lobo aliongea kwa hasira huku akijaribu kuchomoa mikono yake toka kwenye kiti alichokuwa kafungwa barabara na wazee wa kazi wa chumba 123F6.  Hali ya kujikakamua ili atoke pale kwenye kiti, ilifanya mwili wake ututumke na kusambaa misuli kama ananyanyua vitu vizito.
"Mzee Pujini. Fanya yako." Malocha aliongea kumruhusu tena Mzee Pujini aendeleze adhabu zake. Mzee Pujini naye bila kusita, akajaribu moto wake angani kabla hajaanza kazi ya kuchoma ngozi nyeusi ya John Lobo. **** "Hahahahahaa. Kuna muda hamna haja ya kulia bali kucheka kwa sababu maumivu uyapatayo, ni sawa na kukutekenya tu." Sauti ya John Lobo iliongea baada ya Mzee Pujini kumaliza kumchoma kwa gesi maeneo ya ndani ya mapaja na kifuani.
"Look like you are so tough. Lets see. (Unaonekana kama mgumu. Ngoja tuone)." Sauti ya Beda, mshirika au msaidizi wa Mzee Pujini ilisikika ikiongea hayo huku ye' mwenyewe akivaa grovu tayari kutimiza majukumu yake.
Beda akachukua visu fulani vidogo vilivyo kwenye mkoba maalumu kwa ajili ya kuvihifahidhia. Na baada ya kukamata visu hivyo viwili, akawa anavinoa kwa kuvisugulisha vyenyewe kwa vyenyewe huku akitembea mbele ya Lobo huku na huko.
Visu vilivyokuwa vinang'aa kama almasi lakini ni vya siliva, vilipita kifuani mwa Lobo haraka na kuacha alama kama ya X kifuani hapo, na kabla hata Lobo hajalia kwa sababu ya maumivu, akamwagiwa mafuta fulani spesheli ambayo yanauma si kawaida pale yawekwapo kwenye vidonda, lakini ni tiba tosha kwa ambaye anavuja damu.
"Fuc*** you FISSA. And fuc** you all and your mama."Lobo alitukana matusi mazito ya Kimarekani kwa sababu ya maumivu makali yaliyokuwa yanampata kwa wakati ule. Hakika alikuwa katika mateso, lakini bado hakuwa tayari kusema ukweli wowote.
"Lobo. Nia yako ni nini na washirika wako ni wakina nani?" Malocha aliuliza kwa sauti kali tena.
"Nia yangu ni kusafisha pasafi kwa kuweka uchafu. Washirika wangu ni uchafu, umenielewa?." Lobo alijibu kwa hasira kali zilizokuwa zimemjaa moyoni sababu ya kuchanjwa na kuteswa na FISSA.
"Mkuu, niachie mimi nikamuhoji mlemle." Mubarak alitoa ombi ambalo halikukataliwa kwa sababu majibu ya John Lobo yalikuwa hayana mashiko hata kidogo vichwani mwao.
"Ooh! Mubah. Umekuja kuchukua ujumbe wako." Lobo alitoa tabasamu pana baada ya kumuona Mubarak kaingia ndani ya chumba kile.
Mubah hakuongea chochote zaidi ya kuchukua chuma chenye ncha kali kwenye ule mkoba wa kuhifadhia vifaa hivyo vya mateso.
"Nauliza swali. Nataka jibu sahihi." Mubah alimwambia Lobo huku akikaa kwenye kiti ambacho alikivutia mbele ya Lobo. Lobo badala ya kujibu, alitabasamu tena. Tabasamu la kukereketa hata ubongo wa kichaa.
"Mubah. There's two choices. Buy or Sell. (Mubah. Kuna machaguo mawili. Nunua au Uza)" Lobo alimwambia Mubah kwa sauti tulivu. Mubah hakuwa mwenye wasiwasi bali kumtaza John Lobo machoni."The rules of these choices are very simple. (Sheria za haya machaguo ni marahisi sana)" Sauti ya Lobo ilizidi kuchukua nafasi."Acha kazi yako au endelea na kazi yako. Ukiacha kazi, utakuwa umenunua roho za familia yako. Watanusurika na mikono yangu. Ukiendelea na kazi, utakuwa umeniuzia roho za uwapendao. Rahisi sana." Lobo alimaliza kauli yake na hapohapo kwa hasira, Mubah alikandamiza kile chuma chenye ncha kali kwenye paja la Lobo.
Kabla hata Lobo hajakaa sawa kusikilizia yale maumivu, akapokea konde zito la shavu la kushoto hadi damu zikaruka upande mwingine.
Tayari Mubah alikuwa kapandwa na hasira kali ambazo zilimpelekea kusimama na kuanza kumpa mateke mazito John Lobo. Hata pale Malocha alipomuamuru aache anachokifanya, hakusikia lolote bali ngumi na mateke ndivyo aliona ni suluhu tosha kumpunguzia hasira.
Ni Beda na Mzee Pujini ndio walimkamata na kumsogeza pembeni asiendelee kufanya 'unyambirisi' aliokuwa anaufanya.  Kiti alichokuwa kakalishwa Lobo, kilikuwa kimechimbiwa chini hivyo wakati anapigwa alikuwa hadondoki wala kuyumba, hivyo kufanya maumivu kumwingia vilivyo.
"Fpuu." Lobo alitema damu pembeni baada ya Mubah kuwa anasukumwa pembeni.
"Mtoeni nje." Sauti ya kwenye spika ilisikika ikiamuru Mubah atolewe nje.
"Mubah." Lobo alimuita Mubah kabla hajatoka. Mubah akageuka kumuangalia yule mtu aliyemuita.
"Sijabadili maamuzi yangu. Anza kuhesabu sasa, unamasaa ishirini na nne kufanya nilichokwambia. Angalia saa yako, au angalia ile pale." Lobo alimuonesha kwa macho saa iliyokuwa ukutani. Mubah akaiangalia kisha akarudisha macho yake kwa Lobo.
"Tick Tock." Lobo aliongea sauti ya mshale wa saa na kumfanya Mubah ajikurupue toka kwenye mikono ya Mzee Pujini na Beda kwa ajili ya.kwenda kumpa kisago tena Lobo. Lakini hakufanikiwa hilo kwa sababu tayari alikuwa kwenye mikono imara.
"Unafanya nini Mubah." Malocha alimuuliza kwa hasira Mubah baada ya kutolewa katika kile chumba.
"Ni hasira mkuu. Kaniambia maneno ya ajabu sana yule mjinga."
"Hasira za kijinga hizo. Unadhani wakina Beda wangekuwa wanaendekeza hasira kwa kutukanwa na kutishiwa, watuhimiwa wangekuwa wanapona?" Mubah akainamisha kichwa chini na kujiona amekosa mbele ya Mkuu wake.
"Embu twendeni ofisini." Malocha aliamrisha na hakuna aliyekataa kati ya Lisa na Mubah ambao walikuwa kwenye kile kioo wakifatilia mateso ayapatayo Lobo kwa makini na ukaribu.

BAADA YA NUSU SAA.

Ni king'ora kilichokuwepo ndani ya Shirika lile la siri, ndicho kilichowashtua Lisa, Malocha na Mubah waliokuwa ofisini wakijadili njia mbadala za kumfanya Lobo aongee.
Kabla hawajajua sababu ya king'ora hicho kulia, mara mlango wa kioo wa ofisi ya Malocha, aliingia mfanyakazi mmoja akiwa kavaa "headphones" masikioni zilizounganika na kipaza sauti moja kwa moja. Ukimuona ni kama mtangazaiji wa radio fulani, lakini sio.
"Mkuu. Lobo katoroka. Na kawaua Beda na Mzee Pujini." Taarifa hizo zikawakurupua wale vijana wa kazi kwa pamoja na kuanza kuelekea kule walipomuacha John Lobo.
Wakaingia moja kwa moja kwenye kile chumba ambacho walimuacha Lobo, lakini macho yao yalitua kwenye miili ya wachapa kazi wao ikiwa maiti, tena si maiti pekee, bali maiti za kutisha.
 ITAENDELEA


HUYO NDO JOHN LOBO ...USIKOSE SEHEMU YA NNE PAPA HAPA KUENDELEA KUSOMA CHECHE ZA HUYU JAMAA..


Simulizi Mix Entertainment We Touch Your Feelings

0 comments:

Post a Comment