DUKA LA ROHO SEHEMU YA SABA
IMELETWA KWAKO NA SIMULIZI MIX ENTERTAINMENT
MWANDISHI FRANK MASAI
ILIPOISHIA
"Nimekwisha kwambia,
acha hiyo kesi. Ni amri siyo ombi. Nakupa miezi miwili ya kupumzika, utake
usitake, utaenda mapumziko." Malocha ikabidi atumie nguvu za uongozi wake
kuwasilisha hisia zake. Mubah akatulia kwa muda kabla hajarudi kwa yule opareta
na kuchukua ule mkanda wenye tukio zima la siku hiyo.
ENDELEA
"Familia yangu
ipo?" Mubah alimuuliza Malocha kabla hajachukua hatua nyingine kutoka mle
ofisini.
"Nyumba na walinzi
wakiwa na familia yako, vyote vilipigwa kiberiti. Hakuna ambacho kimesalia,
labda majivu." Malocha alimjibu Mubah huku uso wake akiutazamisha mbele na
chozi la kiume likamtiririka jasiri huyu upande wake wa kulia.
"We will be fine
boss. Don't cry sir (Tutakuwa sawa mkuu. Usilie)" Mubah akamwambia mkuu
wake huku akimgonga gonga bega lake kumfariji. Baada ya hapo, akatoka nje ya
ofisi ile na kuelekea kwa Lisa ambaye baada ya kumuona Mubah, alimkimbilia na
kumkumbatia.
"Upo sawa
Mubah." Lisa alimuuliza baada ya kumuachia.
"Nipo sawa Lisa.
Lakini bado sijajua ni vipi Lobo alijua kuwa familia yangu ipo kule."
Mubah alimuuliza Lisa.
"Nadhani kuna kitu
alikiacha katika mwili wa mwanafamilia wako, hicho ndio kilikuwa na GPS ambayo
inaonesha popote waendapo." Lisa akamjibu Mubah na hapo Mubah akakumbuka
kile kibanio kilichokuwa kina sumu hatari kutoka kwenye Yellowstone. Lakini pia
akakumbuka maneno ya mjomba wake kuwa alipewa kibanio na kitu kingine ambacho
yule mjomba hakumalizia kukisema baada ya Mubah kumpora kile kibanio.
"Nadhani itakuwa
hivyo maana kuna sumu waliivuta wale wenzangu wengine, ilitoka kwenye banio
ambalo mimi nilimpora Husna, mjomba wangu. Lakini pia Husna alipewa kitu
kingine na Lobo, nadhani kiliambatana na hiyo GPS. Ila hamna tatizo, naenda
likizo ya miezi miwili, lakini sitalala. Nitakutumia sana kukupa taarifa za
kila upelelezi wangu." Mubah alimwambia Lisa na kisha wakaongea maneno
machache ya kufarijiana kabla Mubah hajachukua jukumu la kwenda chumba cha
mapumziko kilichomo FISSA. ****
"Bado sijaipata mkuu. Na familia yote ya Prince Mubarak imeteketea."
Ni sauti ya Malocha ikiwa inaongea kwenye simu ambayo ilipigwa usiku ule wa saa
tano. Alikuwa rais wa nchi akiulizia ndege kama imepatikana.
"Nasemaje. Mi'
sijali hayo mambo yenu ya kijinga kwenda kukamata mtu mmoja kwa kutumia watu
mia badala ya kufata maelezo ya mtu anachokitaka. Nachotaka mimi hapo ni hiyo
ndege tu! Jumamosi ijayo Rais wa Cuba anakuja, unadhani kuna nini kitatokea kama
hiyo ndege haijapatikana? Naitaka hiyo ndege kabla ya Jumamosi." Rais
akakata simu na kumuacha Malocha akiwa katika wakati mgumu kuliko nyakati zote
ambazo kawahi kuzipitia kimaongezi.
Akiwa na hasira za kuweza
kufanya jambo lolote bila kujizuia, akatoka nje ya ofisi yake na kisha akaita
wafanyakazi wote wa lile shirika.
"Ondokeni wote usiku
huu. Sitaki mtu humu." Malocha aliongea kwa hasira baada ya mjumuiko wa
wafanyakazi wake kuja eneo husika.
"Lakini mkuu, si
ruhusa kuondoka usiku." Mfanyakazi mmoja alikumbusha sheria ya shirika
lao.
"Ninekwishasema.
Lawama zote nitabeba mimi, na si yeyote humu. Poteeni haraka kabla sijafanya
kitu cha ajabu humu." Walimjua Malocha vilivyo, hivyo baada ya kauli ile,
wakazima vitendea kazi vyao na kwenda kwenye usafiri maalumu kwa ajili ya
kuwatoa nje ya shirika lile.
Sasa shirika lote la
kipelelezi likawa limebaki patupu. Hakuna mtu zaidi ya Malocha aliyekuwa
analanda huku na huko akijaribu kutafakari hili na lile kuhusu John Lobo.
"Kanishinda huyu
mbwa. Sina jinsi, inabidi nimtafute tu! Nadhani nitafanikiwa." Yalikuwa
maneno ya Malocha akiongea peke yake. Baada ya maneno hayo, akaenda moja kwa
moja ofisini kwake na kutwaa simu ya mezani, kisha akaifungua na kuweka kitu
fulani ambacho kilisaidia watu wasinase maongezi ambayo watakuwa wanayaongea
kupitia simu hiyo.
"Halo kaka."
Malocha aliitika baada ya simu kupokelewa.
"Vipi Malocha."
Jamaa wa upande wa pili alisalimia.
"John Lobo
karudi." Malocha alimwambia yule jamaa wa pili.
"Mkamateni
sasa." Jamaa akajibu kifupi na kukata simu. Malocha akapagawa kwa kitendo
kile cha jamaa. Hakujua atafanya nini ili kumshawishi yule jamaa amsikilize.
Akatulia kwenye kiti
chake akitafakari njia za kumvuta mtu wake amsikilize. Baada ya dakika kadhaa,
akapata wazo la cha kufanya. Akatwaa simu yake tena na kupiga namba zilezile.
"Usinipigie tena
Malocha." Jamaa alisikika akilalamika kwenye simu.
"Lisa yupo katika
hatari ya kuuawa na Lobo." Malocha akaongea kwa kifupi na kisha akakata
simu. *****
NYUMBANI KWA LISA.
Alifika mida ya usiku
sana na kukuta aishio nao wamekwishalala. Akafungua mlango wa nyumba yake kwa
funguo ambazo anazo na kisha akaingia chumbani kwake ambapo alivua mavazi yake
ya kazi na kuyaweka pembeni. Akavaa mavazi ya kwenda kuogea na baada ya hapo
akaelekea bafuni kujisafi.
Dakika saba za kujisafi
zikatimia, ndipo akatoka akijipukuta na kuelekea katika kitanda ambacho analala
na mume wake Bwana Gunner, jamaa mwenye asili ya Kameruni na Kirusi. Lisa akavuta kipande cha shuka alichojifunika
mumewe na yeye akajifunika tayari kwa kuutafuta usingizi.
"Kazi zako vipi. Na
leo mbona usiku?" Gunner alimuuliza mkewe Lisa.
"Kuna matatizo
makubwa ofisini." Lisa alijibu kimkato na kutulia kabla ya kushtuliwa na
mkono wa Gunner uliopita kiunoni kwake na kumgeuzia upande wake. Wakawa wanabadilishana
pumzi kwa sababu sasa walitazamana.
"Kumetokea
nini?" Gunner akamuuliza Lisa swali ambalo Lisa alilijibu pia kwa kifupi
lakini lilieleza kila kitu ambacho kilitokea.
Baada ya maelezo hayo,
Gunner alimbusu Lisa mdomoni na Lisa naye hakuwa nyuma bali kumpa ulimi kabisa
bwana yule mweusi na aliyejengeka mwili sababu ya mazoezi ayafanyayo.
Baada ya dakika tano, ni
sauti za raha ambazo zilitawala mle ndani. Mabusu motomoto aliyokuwa anayatoa
Gunner kwenda kwa Lisa, hakika yalifaa kuitwa pole yenye raha kwa Lisa. Mtoto
wa kike akawa hoi kabla hata ya mshikemshike wa mapenzi kuanza.
Gunner akazidi kuonesha
utundu wake kwenye mwili wa Lisa. Akabusu la kupitisha ulimi wake huku na huko
hadi pale alipohakikisha mwili wa Lisa upo tepetepe na hoi kwa mambo mazito
ambayo si rahisi kwa msichana wa kileo kuyapokea kwa mwanaume wake. Gunner
akampa mtoto wa kike ile thamani ya ndoa yake, akampa kile ambacho kiukweli
huzidisha hamu ya wapenzi kuwa pamoja. Na zaidi, huongeza chachu ya penzi.
Lisa akajikuta mwenye faraja
mpya baada ya shughuli nzima aliyoifanya mumewe.
Na shughuli kama hiyo
ndio hasa iliyomfanya Lisa asimfiche mumewe ambaye alikuja katika wakati mgumu
alioupitia Lisa. Wakati ambao Lisa alikuwa hana msaada kifikra zaidi ya maumivu
tele baada ya kupotea kwa kipenzi chake Frank Masai na wakati huo anasumbuliwa
na baba yake akiyegundua ujauzito wake.
MIAKA KADHAA NYUMA.
"Lisa. Tumbo lako
limebarikiwa kuliko wanawake wote katika dunia hii. We' ndiye thamani ya moyo
wangu. Hakuna Frank bila Lisa na Lisa bila Frank." Ni sauti ya Frank ikiwa
kitandani pamoja na Lisa ambaye Frank alikuwa akilipapasa tumbo lake.
"Naupenda sana ulimi
wako Man'Sai. Kila mara hunipa faraja ya masikio yangu na kinywa changu."
Lisa akamjibu Frank kwa sauti ya mahaba na kumuongezea busu zito lililoenda
sambamba na kumbate la kushiba.
"Lisa. Nahitaji
tumbo hili libebe kiumbe changu. Upo tayari?" Frank alimuuliza Lisa baada
ya muda mchache wa kumaliza mahaba yao.
"Nakukaribisha
Man'Sai. Sitajutia maamuzi yangu. We' ndiye kila kitu." Maneno hayo
yalimtoka Lisa akiwa kitandani kwa Frank kipindi wapo chuo kikuu mwaka wa
kwanza. Mapenzi yao yalianza tangu
sekondari na muda huo yalikuwa yameshamiri kama maua yaonayo asubuhi au ndege
wa anga wasonapo jua limechomoza.
"Asante Lisa.
Nategemea mwaka wa tatu tutatimiza ndoto hii." Frank akaweka nyongeza
katika maongezi yao.
"Anytime
Man'Sai."
"Thank you
dear." Baada ya maneno hayo, purukushani za mahaba zikapamba moto tena na
kufanya kitanda cha Frank kulalamika kwa kile kinachoendelea. ****
MIAKA MIWILI MBELE.
Ikiwa ndio wanamaliza
chuo, kama kawaida ya Frank na Lisa, wakakutana kimapenzi zaidi lakini wakati
huu walikuwa wanalengo la kusaka mtoto tu! Wiki hiyo wakawa wanakutana kimwili
kila pale walipohitajiana. Lisa akiwa anajua wazi ndani ya wiki hizo ndipo
awezapo kupata ujauzito, akawa haishi miguu yake kwa Frank. Na Frank alionesha
urijali wake kwenye maeneo ya kitandani. Akawa mtu wa kutoa raha kwenda kwa
Lisa na Lisa akitoa raha hizo kwenda kwa Frank.
Baada ya wiki mbili
wakahitimu chuo kikuu. Huo ndio ukawa mwisho wa Frank na Lisa kuonana. Baba
yake Lisa ambaye ni Gavana wa jimbo fulani huko Marekani, akamchukua Lisa kwa
ombi la Rais wa nchi, na kumpeleka chuo cha mafunzo ya Ujasusi. Huko ndipo
ambapo Lisa alipata wasaha wa kujifunza mbinu mbalimbali za kipelelezi na
ujasusi.
Lakini kabla ya kuingia
katika chuo hicho, ilibidi apimwe kwanza afya yake. Hapo ndipo alipogundulika
anaujauzito wa mwezi mmoja. Baba wa Lisa, Mzee Lindsay, aliumia sana kwa
kitendo kile. Ili kuficha aibu ile, akaamua kumtafutia mwanaume mtoto wake
amuoe akiwa na mimba ile.
GUNNER SAMUEL BOKWA.
Kijana mpole na mtulivu katika mambo yake. Anamiliki biashara kadhaa nchini
Marekani, Ufaransa, Urusi na Kameruni alipotokea marehemu baba yake ambaye
ndiye aliyemuachia urithi wa mali zote hizo. Siku zote katika maisha yake
alikuwa ni mtu wa kumsumbua Mzee Lindsay kuhusu mtoto wake. Na baada ya baba wa
Lisa kugundua mwanawake anamimba, akamkimbilia Gunner bila yeye kujua na
kumuomba amuoe mwanaye kabla hajaenda chuo cha ujasusi. Gunner hakuwa na
kipingamizi chochote kwa sababu mapenzi ni upofu. Akamfata Lisa ambaye tumbo
lake bado lilikuwa halijaanza kuchipuka bali uzuri wake ulizidi maradufu.
Gunner akawa boya na
bwege kabisa hasa pale alipopewa ruhusa ya kusadifu umbo mwanana la Lisa likiwa
halina mavazi. Akalichezea wiki nzima kwa mahaba mazito. Mwisho wa yote ukawa
ni harusi kubwa kufungwa katika jiji la Dar es Salaam. Lisa alijitahidi
kuonesha furaha yake, lakini ukweli ni kwamba, hakuwa na furaha hiyo hasa baada
ya kusikia mkasa ambao Frank na Malocha umewakumba kipindi hicho. Mkasa wa Jina
la Chude Bobo. Walikuwa wanatafutwa kama dhahabu machimboni.
ITAENDELEA
KWENDA SEHEMU YA NANE BOFYA HAPA>> SEHEMU YA NANE
0 comments:
Post a Comment