DUKA LA ROHO SEHEMU YA KUMI NA MBILI
IMELETWA KWAKO NA SIMULIZI MIX ENTERTAINMENT
MWANDISHI FRANK MASAI
ILIPOISHIA
"Cha msingi ni wewe
kutulia hapa. Hatofika mtu hapa. Au kama waweza, rudi kwako na kujifanya hujui
lolote. Na kingine, mtoto wako anafundishwa kulenga huku akioneshwa picha ya
Frank." Malocha akamaliza na kuelekea chumba kilichokuwa na mitambo ya
kipelelezi.
Akamuacha Lisa akiwa
kakodoa macho asijue ni nini afanye kwa wakati ule. Mubah naye akanyanyuka na
kuondoka eneo lile akiwa na amani kiasi baada ya Lisa kuugundua ukweli.
ENDELEA
****
Kesho yake asubuhi, Lisa
alikuwa wa kwanza kuamka na kumtazama mwanaye kama kaamka. Alipomuona hajaamka,
akatwaa simu yake ambayo alibadilishiwa na wakina Mubah, kisha akampigia
mumewe.
"Nakuja asubuhi hii
Gunner. Naomba nikukute." Lisa aliongea na upande wa pili ukamjibu. Akamuamsha mtoto wake na kumuuliza maswali
ambayo alikuwa anayauliza Mubah kwenye gari.
"Hiyo picha ambayo
anakuonesha, yupoje huyo mtu." Swali mojawapo la Lisa kwenda kwa Martina.
"Mweusi hivi, mrefu
kiasi halafu ananywele za kung'aa na nyeusi." Martina alimjibu Lisa majibu
ambayo yalimfanya apumue kwa shida.
"Okay. Basi twende
nyumbani kwa baba eeeh. Leo tutamuaga na kuja kukaa huku. Si ndio eeh."
Lisa akamwambia mwanaye huku akijitahidi kuchongesha tabasamu.
"Haya mama."
Martina alijibu kwa furaha hasa kwa sababu atakuwa karibu na mama yake kuliko
kipindi chochote cha maisha yake. **** "Nitakuwa nyumbani tu leo,
sitaondoka kabisa." Lisa alikuwa anamwambia Gunner huku akiwa katabasamu
kana kwamba hajui kitu.
Alishaondoka Kivule na
sasa alikuwa uso kwa uso akitazamana na Gunner.
"Okay. Basi mimi
naelekea ofisini. Nitarudi usiku leo." Gunner aliongea na kumpa busu dogo
mke wake. Akatoka nje na kuondoka.
BAADA YA SAA MOJA.
Lisa alikuwa akitupia
nguo zake haraka haraka kwenye begi lake kwa lengo la kuondoka katika nyumba
ile. Akafanikiwa hilo na hata kuandika ujumbe ambao atauacha mezani baada ya
kuondoka.
Akanyanyua begi lake
tayari kwa kutoka nje ya chumba chake. Akatoka na kuanza kuelekea sebuleni huku
akiita jina la Martina.
"Una safari mke
wangu." Macho ya Lisa hayakuamini pale alipomkuta Gunner kakaa sebuleni na
Martina ambaye alikuwa hana habari wala kuhisi kitu kibaya. Lisa akashindwa
kujitetea na badala yake akawa anatetemeka huku akimuangalia mwanaye ambaye Gunner
alikuwa akizilaza nywele zake kwa taratibu.
Gunner akanyanyuka pale
kochini na kumfuata Lisa kisha akampora karatasi aliyokuwa kaikamata. Ni ujumbe
ambao alikuwa kauandika Lisa na alitaka kuuacha mezani kabla hajaondoka.
"Kwa hiyo umekwisha
nifahamu. Safi sana. Ndivyo mpelelezi unavotakiwa kuwa." Gunner aliongea
hayo baada ya kuusoma ule ujumbe. Hakuishia hapo yule mwanaume, akaongea kwenye
kinasa sauti alichokuwa kakivaa na baada ya dakika mbili akaingia msichana
ambaye Martina alipomuona alimkimbilia na kumkumbatia kwa furaha akimuita mama
mdogo.
Lisa alikuwa katoa macho
asiamini kile anachokiona mbele yake. Ni mzimu au nini? "Huyu ndiye
ulikuwa ukipambana naye jana Lisa." Gunner aliongea kwa utaratibu kama
kawaida yake.
"Zakia!?" Lisa
akaita kwa mshangao asiamini kile akionacho.
"Ndiye mimi Lisa.
Mchumba wa Mubarak. Prince Mubarak au Mubah." Mtu aliyeitwa Zakia alijibu
kwa nyodo nyingi huku akimpapasa Martina kwa upendo.
"Kweli jambo
usilolijua, ni sawa na usiku wa kiza. Malocha aliongea haya hapo jana."
Lisa akajikuta akiropoka.
?Kuna muda unatakiwa
kutambua kuwa hakuna siri inayodumu katika moyo wa mtu. Ukikuta siri imedumu
baina yenu wawili, basi ujue ipo karibuni kuvunjika.
Umenificha jambo dogo
sana Lisa. Na kila siku nilikuwa nasubiri ulitamke, lakini ulishindwa
kuniambia. Sijui ni mke wa aina gani wewe." Gunner alikuwa anaongea kwa
makini hasa akitaka Martina asiyasikie yale maongezi."Baada ya kujua kuwa
sina uwezo wa kuzalisha, nikatafuta ukweli juu ya hiki kijimtu nachokilea.
Kishetani kipya, kidogo-dogo." Gunner alinyoosha kidole kwa Martina wakati
anaropoka maneno haya.
"Usimuite mwanangu
hayo majina we' mshenzi mkubwa." Lisa naye kwa umakini alijikuta
akimkaripia Gunner.
"Nikafatilia kwa
makini sana kuhusu hiki kishetani, ni cha nani? Ndipo nikapekua vitu vyako na
kukuta ile picha aliyokuonesha Kamanda Lobo. Hapo ndipo nikajua kishetani baba
yake ni yule mbwa muoga. Mbwa anayeogopa kurudi nchini kwao na kulowea nchi za
watu. A coward." Lisa alijikuta akijawa na hasira na kurusha mkono wake
lakini Gunner aliudaka vema na kumkamata Lisa kiuno wakawa kama wachezao nyimbo
za taratibu.
"Baada ya kugundua
kuwa ni mtoto wa yule muoga au mzamiaji, nikaamua kuutafuta ukweli zaidi.
Nikamfuata baba yako na kumuuliza kuhusu hali ile." Gunner alikuwa akiongea
taratibu huku bado kamkamata Lisa kiuno na kucheza naye blues.
"Jinsi baba yako
alivyokuwa mjinga, akaanza kuniomba msamaha kama vile mimi ni MUNGU. Lakini kwa
bahati mbaya, alinikuta si mimi yule niwezaye kucheka kama katuni. Akanikuta ni
Gunner mwingine kabisa. Kwa hii mikono yangu." Gunner akamuachia Lisa na
kukunja mikono yake hadi misuli kadhaa ikatutumka na kumuonesha ukubwa wa mwili
wake. "Nikamnyonga baba yako hadi akafa hapo hapo. Hiyo ndiyo ikawa ahueni
kwangu Lisa, nikapunguza hasira zangu kihivyo." Gunner alimaliza akiwa na
tabasamu pana kana kwamba kile akiongeacho ni kitamu sana kukimeza.
"Martina. Nenda na
mama mdogo kule nyumba nyingine, mimi nitakuja na mama eeh."Gunner
alimwambia Martina ambaye hakupinga lolote bali kujawa na furaha hasa kwa kuwa
huko kuna raha na starehe za kila aina kwa watoto.
"Bayi mama."
Martina alimuaga mama yake huku akiwa na furaha tele.
"Muage mtoto wako
Lisa." Gunner akamnong'oneza Lisa lakini Lisa hakufanya chochote zaidi ya
kupumua kwa kasi kutokana na hasira zilizojishindilia akilini mwake.
"Kama hutaki, basi.
Muache aende." Lisa akashuhudia mwanaye anaondoka bila kuaga.
"We mshenzi kumbe
ndiye uliyemuua baba yangu." Lisa akamsukuma Gunner aliyekuwa akicheka kwa
nyodo kutokana na hali ambayo Lisa alikuwa nayo.
"Tena baada ya
kumuua, tukavumisha kiharusi ndicho kilichombeba yule Mmarekani. Pesa tu."
Gunner akazidi kumjaza hasira Lisa.
Lisa akaanza kumpiga
ngumi nyingi kila mahali mwanaume yule lakini ngumi zile zilikuwa kama kumpiga
mwizi kwa ndala, hazimuumizi.
Lisa akajikuta akiishiwa
nguvu sababu ya hasira na hizo ngumi alizokuwa anazitupa.
"Umemaliza
wife?" Gunner aliuliza huku akiwa anatabasamu pana usoni pake. "Okay.
Sasa ni muda wa wewe kwenda kumsalimu baba yako huko kuzimu. Nadhani kakumiss
sana." Gunner akaongeza huku akianza kumufata taratibu Lisa ambaye naye
alianza kusogea nyuma huku akitetemeka na maneno ya Malocha yakamrudia kichwani
kuwa ni heri akutane na treni ya umeme relini kuliko kukutana na sura halisi ya
Gunner.
Mwisho wa safari ya Lisa
ilikuwa ni kugota ukutani ambapo alishindwa kwenda zaidi nyuma.
"Midomo yako, ni
midomo ambayo nilienjoy sana pale nilipokuwa nainyonya. Ni milaini na inatoa
sauti mororo pale inapokutana na kitu kitamu. Mmmh! You're so sweet my sweet
Lisa." Maneno hayo yaliongozana na mkono wa kuume wa Gunner kushika midomo
hiyo mwanana ya kiumbe Lisa.
Hakuishia hapo, akashuka hadi kifuani na
kuanza kuminya matiti murua na yenye mvuto aliyobarikiwa kuumbwa nayo Lisa.
"Hapa ndipo ubovu
wangu ulipo, always nilijihisi mwenye bahati kula mbivu kama hizi. Hakika
zilinipeleka katika sayari nyingine ya mahaba. Kama usingekuwa na kosa hili
ulilolifanya, ningeendelea kula kifua hiki mwanana." Akatoka kifuani
Gunner na kuhamia katika kiuno chembamba na kilichojichimbia ndani kiasi na
kisha kuibuka tena kwa chini kwa shepu matata.
"Oooh Lisa.
Unanichanganya na hichi kiuno chako hasa pale kinapozunguka katika maumbile
yangu. Ulinichanganya kwa kila hila we' mwanamke. Kiuno chako hakifiki kwa yule
Waziri malaya wa Wanawake. Alikuwa anajitahidi sana kukilandisha, lakini ni
kama kabanwa na plaizi ya kiuno. Kiuno kigumu kama kinu." Gunner akacheka
sana kutokana na maneno hayo. Akaendelea,
"Najua utashangaa,
lakini ndivyo ilivyo. Nilikuwa nachepuka naye mara kwa mara kwa sababu ya
miradi anayomiliki. Lakini alifanya kosa moja tu! Ndilo lilimpeleka kaburini
mpumbavu yule.
Sijui alitumwa na nani
kunichunguza. Akakosea akagusa pasipogusika. Nikampa roho yake Lobo. Na Lobo
hafanyi makosa, akampa masaa. Akashindwa kutimiza kuachia madaraka na kuondoka
nchini. Roho yake ikawa yetu baada ya kushindwa kuinunua." Gunner alizidi
kumtisha Lisa ambaye alikuwa anatetemeka kama mwenye ugonjwa wa tetenasi.
ITAENDELEA
KWENDA SEHEMU YA KUMI NA TATU BOFYA HAPA=>SEHEMU YA KUMI NA TATU
0 comments:
Post a Comment